About Us   |   Contact Us   |  
Submission  

Wahusika wa Riwaya za Kimajaribio: Uchunguzi wa Maana Fiche Katika Riwaya ya Nagona

DOI : https://doi.org/10.36349/easjehl.2026.v09i08.001
PDF
HTML
XML

Riwaya ya kimajaribio imekuwa na ugumu wa usimbuaji wa maana. Hali hii inatokana na riwaya hizi kuhusisha vipengele vingi vilivyo chagamani. Aidha, vipengele hivi vimekuwa vichocheo vya kujenga maana fiche. Miongoni mwa kipengele cha msingi cha kisanaa katika ujenzi wa maana fiche ni wahusika. Nagona ni riwaya ya kimajaribio iliyotumia kipengele cha wahusika kwa umahiri ili kuficha maana ndani yake. Data za utafiti huu zilizokushanywa maktabani kwa mbinu ya usomaji makini. Uchambuzi wake ulitumia Nadharia ya Semiotiki kupitia msimbo wa kiishara. Matokeo yanaonesha kuwa, riwaya ya Nagona imetumia wahusika wa kiitikadi, wahusika jumui na wahusika wa kisasili katika kujenga maana fiche. Wahusika wa kiitikadi wanadokeza kuhusu Nabii na Mtume kama wajumbe waliokuja na neno lenye uhusiano kutoka kwa Mungu mmoja. Pia, wanaonesha kuwa, wanafalsafa wa kidunia wamekuwa ni kikwanzo cha kufikia ukweli wa imani juu ya Mungu wa mbingu na aridhi. Wahusika jumii wanadokeza viongozi wa kijamii wanavyoshiriki katika kuendeleza ukoloni mamboleo katika jamii zao. Ama wahusika wa kisasili wanadokeza dhana ya ukweli, elimu na mji mtukufu ambao umekuwa na utata kuhusu nani anahaki zaidi ya kuumiliki. Wahusika hawa wamesawiriwa katika misingi ya kidhanaishi kutokana na mwingilianomatini katika vitabu vitakatifu vya Qur-ani na Biblia. Kutokana na hali hiy, maana nyingi zimejikita katika masuala ya kidini pamoja na nadharia za wanafalsafa. Makala hii inapendekeza kufanyika tafiti zaidi katika suala la kuangalia mitindo iliyotumika kusawiri wahusika wa kazi hizo. Pia, kutafiti ulinganashi wa usawiri wa wahusika katika kazi za mwandishi Kezilahabi na waandishi wengine wa kimajaribio.

TOP EDITORS

OPEN ACCESS JOURNALS

Professor Thomas Count Dracula, MD, PhD

Distinguished Professor of Haematology Head — Experimental, Historical & Sensory Haematology Vlad the Impaler University, Wolf’s Lane, Wooden Stakes Grove 666, Transylvania.

BEST AUTHOR

Of The Month

TRACK YOUR ARTICLE

Enter the Manuscript Reference Number (MRN)
Get Details

Contact us


EAS Publisher (East African Scholars Publisher)
Nairobi, Kenya


Phone : +91-9365665504
Whatsapp : +91-8724002629
Email : easpublisher@gmail.com

About Us


EAS Publisher (East African Scholars Publisher) is an international scholar’s publisher for open access scientific journals in both print and online publishing from Kenya. Its aim is to provide scholars ... Read More Here

*This work is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial 4.0 International License.

© 2020, All Rights Reserved | SASPR Edu International Pvt. Ltd.

Developed by JM