About Us   |   Contact Us   |  
Submission  

Ubainishaji wa Vipengele vya Ujumi wa Kiafrika na Athari yake katika Ushairi wa Kiswahili: Uchunguzi wa Ushairi wa Bongo Fleva

DOI : https://doi.org/10.36349/easjehl.2026.v09i03.005
PDF
HTML
XML

Makala haya yalichunguza ujitokezaji wa ujumi wa Kiafrika katika ushairi wa Kiswahili wa Bongo Fleva pamoja na athari yake katika ushairi huo. Tafiti kuhusu vipengele vya ujumi wa Kiafrika zimeishia katika kubainisha ujitokezaji wake pasi na kuonesha athari (matokeo) yake katika kazi husika. Hali hii inachangia kutobaini umuhimu wa ujumi huo katika kazi za kifasihi za jamii ya Kiafrika jambo linalochangia baadhi ya kazi za kifasihi kutokusawiriwa vyema katika jamii. Data za makala haya zilipatikana katika maktaba ya kidijiti kwa kutazama na kusikiliza mashairi ya Bongo Fleva kisha kuchambua ujitokezaji wa ujumi wa Kiafrika na athari yake katika ushairi huo. Njia hii ilitumika kwa sababu njia nyingine za ukusanyaji wa data zisingeweza kuzifikia data zinazopatikana katika maktaba ya mtandaoni. Uchambuzi wa data za makala hii uliongozwa na Nadharia ya Ujumi Mweusi. Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa, ujumi wa Kiafrika katika ushairi wa Bongo Fleva una athari kubwa katika ushairi huo. Athari hiyo imebainika kusababishwa na usawiri kwa mawanda mapana vipengele vya Ujumi wa jamii wa Kiafrika ambavyo ni umoja na ushirikiano, ushababi, matumizi ya lugha za Kiafrika katika kukuza ama kubomoa kazi ya kifasihi, matumizi ya mazingira halisi ya jamii za Kiafrika pamoja na kipengele cha utu na ukarimu. Vipengele hivyo vimekuwa na athari (matokeo) kama vile kujenga diplomasia ya kisanaa baina ya mataifa ya Kiafrika, kuibua utalii wa ndani na nje ya Tanzania, kujenga umoja wa kisanaa baina ya wasanii ndani na nje ya Tanzania pamoja na kuleta umajumui wa kibara katika sanaa. Kwa muktadha huo, wasanii wanashauriwa kuendelea kutunga nyimbo zenye kusawiri ujumi wa Kiafrika kwa mawanda mapana. Hali hii itasaidia kazi za kifasihi za jamii mahususi (ikiwemo ushairi wa Bongo Fleva) kupata ukubalifu katika jamii kwa urahisi kuliko ingekuwa vinginevyo.

TOP EDITORS

OPEN ACCESS JOURNALS

Professor Thomas Count Dracula, MD, PhD

Distinguished Professor of Haematology Head — Experimental, Historical & Sensory Haematology Vlad the Impaler University, Wolf’s Lane, Wooden Stakes Grove 666, Transylvania.

BEST AUTHOR

Of The Month

TRACK YOUR ARTICLE

Enter the Manuscript Reference Number (MRN)
Get Details

Contact us


EAS Publisher (East African Scholars Publisher)
Nairobi, Kenya


Phone : +91-9365665504
Whatsapp : +91-8724002629
Email : easpublisher@gmail.com

About Us


EAS Publisher (East African Scholars Publisher) is an international scholar’s publisher for open access scientific journals in both print and online publishing from Kenya. Its aim is to provide scholars ... Read More Here

*This work is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial 4.0 International License.

© 2020, All Rights Reserved | SASPR Edu International Pvt. Ltd.

Developed by JM