About Us   |   Contact Us   |  
Submission  

Mbinu Zinazotumika Kuunda Motifu za Safari na Msako Katika Mashairi ya Kimaelezo: Mifano Kutoka Katika Diwani ya Sauti ya Dhiki (1973) ya Abdilatif Abdalla

DOI : https://doi.org/10.36349/easjehl.2025.v08i12.001
PDF
HTML
XML

Makala hii inahusu mbinu zilizotumika kuunda motifu za safari na msako katika mashairi ya Kiswahili katika diwani ya Sauti ya Dhiki (1973) ya Abdilatif Abdalla. Makala hii inalenga kuiziba pengo la kiutafiti juu ya mbinu zinazounda motifu, kwani hakuna tafiti zilizofanyika kubainisha mbinu zinazounda motifu za safari na msako katika Ushairi. Katika uga wa fasihi baadhi ya wataalamu wamechambua mbinu mbalimbali za kisanaa zinazounda kazi za fasihi kwa ujumla, na wale walioangalia muundo wa motifu katika kazi za fasihi walibaini hisia ndio kichocheo kikuu kinachosababisha ujirudiajirudiaji wa kimotifu, hivyo basi hisia huunda motifu. Ushairi wa kimaelezo ni miongoni mwa kazi za fasihi zilizo na motifu za safari na msako na zinaundwa kwa miundo bayana. Licha ya tafiti mbalimbali kubaini kwamba motifu hizo zinajitokeza zaidi katika ushairi simulizi na ule wa kidrama. Ombwe la tafiti juu ya mbinu zinazotumika kuunda motifu za safari na msako limekuwa bayana hususani katika mashairi ya kimaelezo. Hali hii ikiachwa bila kuchunguzwa inasababisha kukosekana kwa maarifa kuhusu mbinu zinazotumika kuunda motifu hususani motifu za safari na msako katika mashairi ya kimaelezo. Mashairi ya kimaelezo yaliyorejelewa ni yale yanayopatikana katika diwani ya Sauti ya Dhiki (1973) ya Abdilatif Abdalla. Data za Makala hii zilikusanywa kwa kutumia mbinu ya usomaji makini wa matini teule wa mashairi ya kimaelezo katika diwani teule. Nadharia za Mwingilianomatini na Ruwaza ya Shujaa ndizo zilizoongoza ukusanyaji na uchambuzi wa data za Makala hii kupitia misingi yake mbalimbali kama itakavyofafanuliwa katika Makala. Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa kuna mbinu tano zilizobainika kuunda motifu za safari na msako katika mashairi ya kimaelezo katika diwani teule. Mbinu hizo ni mbinu ya ruwaza, mbinu ya diolojia, mbinu ya shajara, mbinu ya kisitiari na mbinu ya sauti ya usimulizi.

TOP EDITORS

OPEN ACCESS JOURNALS

Professor Thomas Count Dracula, MD, PhD

Distinguished Professor of Haematology Head — Experimental, Historical & Sensory Haematology Vlad the Impaler University, Wolf’s Lane, Wooden Stakes Grove 666, Transylvania.

BEST AUTHOR

Of The Month

TRACK YOUR ARTICLE

Enter the Manuscript Reference Number (MRN)
Get Details

Contact us


EAS Publisher (East African Scholars Publisher)
Nairobi, Kenya


Phone : +91-9365665504
Whatsapp : +91-8724002629
Email : easpublisher@gmail.com

About Us


EAS Publisher (East African Scholars Publisher) is an international scholar’s publisher for open access scientific journals in both print and online publishing from Kenya. Its aim is to provide scholars ... Read More Here

*This work is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial 4.0 International License.

© 2020, All Rights Reserved | SASPR Edu International Pvt. Ltd.

Developed by JM