About Us   |   Contact Us   |  
Submission  

Uchambuzi wa Ujumi katika Muziki wa Benga wa Jamii ya Wakamba: Mkabala wa Umtindo

DOI : https://doi.org/10.36349/easjehl.2025.v08i09.009
PDF
HTML
XML

Muziki wa Benga ni utanzu maarufu nchini Kenya. Hujitambulisha kwa sifa ya mdundo na mapigo ya kasi pamoja na ustadi wa msanii wa kucheza gitaa na kuimba kwa mtindo maalum. Licha ya ustadi wa matumizi ya mtindo katika muziki wa Benga wa jamii ya Wakamba, bado kuna pengo la kitaaluma kuhusiana na uchanganuzi wa kina wa jinsi vipengele vya mtindo katika muziki huu vinavyotumika kuimarisha ujumi. Utafiti huu ulilenga kuchanganua namna mikakati ya mtindo inayotumika katika muziki huu inavyoimarisha ujumi na athari za kijamii. Uchunguzi huu uliongozwa na kielelezo cha nadharia ya Umtindo. Umtindo hufasiri na kuhakiki tungo kwa kuzingatia mtazamo wa kiisimu kama taaluma iliyo na uhusiano wa karibu na fasihi. Uchunguzi wa kimtindo huhusisha namna lugha inavyotumika katika matini ili kujenga maana na athari. Usampulishaji ulifanywa kimakusudi ambapo nyimbo za muziki wa Benga wa jamii ya Wakamba ziliteuliwa. Ukusanyaji wa data ulihusisha upakuaji wa nyimbo za Benga kutoka kwa mtandao wa kijamii wa Youtube na unakili wa mishororo yake. Mbinu ya uchanganuzi matini ilitumika kubainisha mikakati ya kimtindo na kuchanganuliwa kimaelezo kwa kuelekezwa na mihimili ya nadharia ya umtindo. Data zilikuwa ni maneno, dhana, kauli, virai na sentensi zinazotumiwa na waimbaji wa muziki wa Benga wa jamii ya Wakamba zinazohusisha vipengele vya kimtindo. Utafiti uliweza kubaini kuwa waimbaji hao hutumia vipengele vya kimtindo kuimarisha ujumi wa kihalisia, kigothiki, kimapenzi, kisiasa, kitamaduni na ujumi wa kiishara. Utafiti huu unasisitiza uhusiano thabiti baina ya muziki, utamaduni na lugha katika jamii, ukionyesha dhima ya ujumi katika kuwasilisha ujumbe kwa jamii. Utafiti huu ni muhimu katika kuufanya muziki wa Benga wa jamii ya Wakamba kutambulika katika nyanja za utafiti wa kielimu wa fasihi na lugha kama kategoria ya nyimbo za kitamaduni. Utachangia taaluma ya isimu na mawasiliano.

TOP EDITORS

OPEN ACCESS JOURNALS

Professor Thomas Count Dracula, MD, PhD

Distinguished Professor of Haematology Head — Experimental, Historical & Sensory Haematology Vlad the Impaler University, Wolf’s Lane, Wooden Stakes Grove 666, Transylvania.

BEST AUTHOR

Of The Month

TRACK YOUR ARTICLE

Enter the Manuscript Reference Number (MRN)
Get Details

Contact us


EAS Publisher (East African Scholars Publisher)
Nairobi, Kenya


Phone : +91-9365665504
Whatsapp : +91-8724002629
Email : easpublisher@gmail.com

About Us


EAS Publisher (East African Scholars Publisher) is an international scholar’s publisher for open access scientific journals in both print and online publishing from Kenya. Its aim is to provide scholars ... Read More Here

*This work is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial 4.0 International License.

© 2020, All Rights Reserved | SASPR Edu International Pvt. Ltd.

Developed by JM