About Us   |   Contact Us   |  
Submission  

Changamoto za Upimaji Jumuishi katika Ufundishaji wa Kiswahili kama Lugha ya Kigeni

DOI : https://doi.org/10.36349/easjehl.2025.v08i06.012
PDF
HTML
XML

Upimaji wa Kiswahili kama lugha ya kigeni umekuwa ukifanyika kwa namna tofautitofauti. Mathalani, upimaji unaojumuisha stadi zote za lugha na upimaji unaozingatia baadhi ya stadi za lugha na kuziacha nyingine. Nadharia Jumuishi ya Lugha inasisitiza upimaji unaojumuisha stadi zote za lugha ili kupata picha halisi ya mafanikio ya mjifunzaji. Licha ya kuwapo kwa tafiti mbalimbali zinazoangazia upimaji wa Kiswahili kama lugha ya kigeni, tafiti hizo hazioneshi changamoto zinazoukabili mchakato wa upimaji kiasi cha kutofautiana kwa kuzingatia au kutozingatia maelezo ya kinadharia. Makala hii imechunguza changamoto za upimaji jumuishi wa stadi za lugha katika ufundishaji wa Kiswahili kama lugha ya kigeni nchini Tanzania. Data za makala hii zilikusanywa kwa kutumia mbinu ya uchambuzi wa nyaraka na usaili. Jumla ya walimu kumi na wawili (12) wanaofundisha Kiswahili kama lugha ya kigeni kutoka katika vituo vitatu (3) walihusika katika utafiti huu. Data zilichambuliwa kwa kutumia mbinu ya uchambuzi wa data kimaudhui ikiongozwa na Nadharia ya Usababishi iliyoasisiwa na Hume (1739) na kuboreshwa (1748). Matokeo ya utafiti yalibaini changamoto mbalimbali zinazokabili upimaji jumuishi wa stadi za lugha. Changamoto hizo ni: kutofautiana kwa malengo ya wajifunzaji wa lugha, kutofautiana kwa miongozo ya ufundishaji, kukosekana kwa mwongozo rasmi wa Upimaji wa Kiswahili kama lugha ya kigeni, mkazo wa stadi za lugha katika ufundishaji na upimaji, ugumu wa upimaji jumuishi wa stadi zote za lugha na matumizi ya uzoefu binafsi. Kutokana na matokeo hayo, utafiti huu unajenga hoja kuwa kuna haja ya kuweka mikakati ili kuboresha zaidi upimaji jumuishi katika ufundishaji wa Kiswahili kama lugha ya kigeni.

TOP EDITORS

OPEN ACCESS JOURNALS

Dr. Afroza Begum

Lecturer, Dept. of Pharmacology and Therapeutics, Shaheed Monsur Ali Medical College & Hospital, Uttara, Dhaka-1230, Bangladesh

BEST AUTHOR

Of The Month

TRACK YOUR ARTICLE

Enter the Manuscript Reference Number (MRN)
Get Details

Contact us


EAS Publisher (East African Scholars Publisher)
Nairobi, Kenya


Phone : +91-9365665504
Whatsapp : +91-8724002629
Email : easpublisher@gmail.com

About Us


EAS Publisher (East African Scholars Publisher) is an international scholar’s publisher for open access scientific journals in both print and online publishing from Kenya. Its aim is to provide scholars ... Read More Here

*This work is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial 4.0 International License.

© 2020, All Rights Reserved | SASPR Edu International Pvt. Ltd.

Developed by JM