About Us   |   Contact Us   |  
Submission  

Ubainishaji wa Dhima Zilivyojitokeza Kupitia Vipengele vya Ushikamani wa Darajia ya Kisarufi Kupitia Tamthiliya ya Natala na Morani

DOI : https://doi.org/10.36349/easjehl.2024.v07i12.007
PDF
HTML
XML

Makala hii imebainisha dhima zilivyojitokeza kupitia vipengele vya ushikamani wa darajia ya kisarufi katika tamthiliya ya natala (Kithaka Wa Mberia, 1997) na morani (Emanuel Mbogo, 1993). Makala hii yalitumia mkabala wa kimaelezo na usampulishaji lengwa. Usanifu unahusu tafiti zinazolenga kuchunguza jambo fulani kwa kina. Data zilikusanywa kutoka maktabani kwa kutumia mbinu ya uchanganuzi matini na kuchambuliwa kwa kutumia mbinu ya kusimbisha maudhui. Mjadala wa matokeo ya utafiti uliongozwa na nadharia ya Ushikamani iliyoasisiwa na Halliday na Hassan (1976). Hivyo matokeo ya makala yalionyesha kuwa matini na kazi mbalimbali za kifasihi huweza kuwa na ushikamani wa mawazo endapo vipengele vya darajia ya ushikamani wa kisarufi vitazingatiwa na kufuatwa, ili ziweze kuwa na ushikamani wenye kuleta mtiririko mzuri wa mawazo. Hata hivyo katika upande wa dhima za darajia ya ushikamani wa kisarufi matokeo yalionesha kuwa dhima hizi zinasaidia kuleta mtiririko wa matini ambao ni wa kueleweka kwa wasomaji au wasilikilizaji (Halliday na Hassan, 1976). Kwa hiyo matini haiwezi kuwa matini bila ya sentensi zake kushikamana sawasawa. Hivyo darajia ya ushikamani ni nguzo katika kazi za fasihi kwani huleta mtiririko mzuri wa mawazo kwa kuwa kazi nyingi zikikosa ushikamani zinakosa maana iliyokusudiwa.

TOP EDITORS

OPEN ACCESS JOURNALS

Dr. Afroza Begum

Lecturer, Dept. of Pharmacology and Therapeutics, Shaheed Monsur Ali Medical College & Hospital, Uttara, Dhaka-1230, Bangladesh

BEST AUTHOR

Of The Month

TRACK YOUR ARTICLE

Enter the Manuscript Reference Number (MRN)
Get Details

Contact us


EAS Publisher (East African Scholars Publisher)
Nairobi, Kenya


Phone : +91-9365665504
Whatsapp : +91-8724002629
Email : easpublisher@gmail.com

About Us


EAS Publisher (East African Scholars Publisher) is an international scholar’s publisher for open access scientific journals in both print and online publishing from Kenya. Its aim is to provide scholars ... Read More Here

*This work is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial 4.0 International License.

© 2020, All Rights Reserved | SASPR Edu International Pvt. Ltd.

Developed by JM