About Us   |   Contact Us   |  
Submission  

Athari za Urazinishaji wa Wahusika Watoto katika Filamu za Kiswahili

DOI : https://doi.org/10.36349/easjehl.2024.v07i12.003
PDF
HTML
XML

Makala hii inahusu athari za urazinishaji wa wahusika watoto katika filamu za Kiswahili. Tafiti za kifasihi na kisaikolojia zinazohusiana na masuala ya watoto katika nyuga mbalimbali zinaonesha kuwa watoto wana urazini wa hali ya juu ikilinganishwa na umri wao. Katika uga wa fasihi, baadhi ya wataalamu wanabainisha kuwa urazinishaji wa wahusika watoto katika kazi za fasihi kama vile tamthiliya na vichekesho unabainika kutokana na matendo na lugha wanayotumia kuwa juu ya urazini wao. Filamu ni miongoni mwa kazi za fasihi zinazotumia wahusika watoto na hupendwa na hadhira pana ya watoto. Kwa hiyo, ni rahisi kwa wahusika watoto kujifunza mambo ambayo wakati fulani huwa nje ya uelewa wao na umri wao. Licha ya watoto kujifunza mambo yaliyo nje ya uwezo wao, bado uchunguzi kuhusu urazinishaji wa wahusika watoto katika filamu za Kiswahili haujapewa kipaumbele. Hali hii ikiachwa bila kuchunguzwa inasababisha kukosekana kwa maarifa kuhusu athari za urazinishaji kwa wahusika watoto katika filamu za Kiswahili. Filamu zilizorejelewa ni za Steven Kanumba zilizotumia wahusika watoto. Filamu hizo ni Ripple of Tears, (2010), This Is It (2010), Uncle JJ (2010) na Big Daddy (2010). Data za makala hii zilikusanywa kwa kutumia mbinu ya usaili kutoka kwa wahusika waliokuwa watoto katika filamu hizo (kwa sasa ni vijana), wazazi wa wahusika hao na mtunzi wa filamu hizo. Nadharia ya Saiko-Changanuzi iliyoasisiwa na mwanasaikolojia wa Kiswisi, Sigmund Freud (1856-1939) ndiyo iliyoongoza ukusanyaji na uchambuzi wa data za makala hii kupitia msingi wa ung’amuzi bwete. Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa kuna athari chanya na hasi za urazinishaji wa wahusika watoto kupitia filamu za Kiswahili. Athari chanya ni kukuza uwezo wa kufikiri kwa mhusika mtoto, chanzo cha kipato kwa mtoto na familia yake, hadhira ya watoto kuiga fanani ambaye ni mhusika mtoto. Aidha, athari hasi ni pamoja na athari za kisaikolojia, mhusika mtoto kujengewa mtazamo hasi kwenye jamii, changamoto za ukuaji kutoka ...

TOP EDITORS

OPEN ACCESS JOURNALS

Dr. Afroza Begum

Lecturer, Dept. of Pharmacology and Therapeutics, Shaheed Monsur Ali Medical College & Hospital, Uttara, Dhaka-1230, Bangladesh

BEST AUTHOR

Of The Month

TRACK YOUR ARTICLE

Enter the Manuscript Reference Number (MRN)
Get Details

Contact us


EAS Publisher (East African Scholars Publisher)
Nairobi, Kenya


Phone : +91-9365665504
Whatsapp : +91-8724002629
Email : easpublisher@gmail.com

About Us


EAS Publisher (East African Scholars Publisher) is an international scholar’s publisher for open access scientific journals in both print and online publishing from Kenya. Its aim is to provide scholars ... Read More Here

*This work is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial 4.0 International License.

© 2020, All Rights Reserved | SASPR Edu International Pvt. Ltd.

Developed by JM