About Us   |   Contact Us   |  
Submission  

Matumizi Ya Lakabu Za Wanafunzi Kama Mkakati Wa Kurahisisha Ufundishaji Na Ujifunzaji Wa Kiswahili Kama Lugha Ya Kigeni Nchini Tanzania

DOI : https://doi.org/10.36349/easjehl.2024.v07i11.006
PDF
HTML
XML

Miongoni mwa sehemu ambazo lakabu hutumika ni katika ufundishaji na ujifunzaji wa lugha ya kigeni (Lgn). Matumizi hayo yameibua maswali kuhusu mchango unaotokana na matumizi ya lakabu katika ufundishaji wa lugha ya kigeni. Tafiti mbalimbali zimefanyika kuhusu matumizi ya lakabu katika ufundishaji wa Lgn lakini hakuna utafiti uliochunguza kama matumizi ya lakabu yanachangia kurahisisha ufundishaji na ujifunzaji wa lugha ya kigeni. Suala hilo limeacha maswali kuhusu mchango wa matumizi ya lakabu katika kurahisisha ufundishaji na ujifunzaji wa Lgn. Makala hii imebaini namna lakabu zinavyotumika kurahisisha ufundishaji na ujifunzaji wa Kiswahili kama Lgn. Data hiyo imepatikana kwa kuchunguza ni kwa namna gani lakabu za wanafunzi zinatumiwa kama mkakati wa kurahisisha ufundishaji na ujifunzaji wa Kiswahili kama Lgn nchini Tanzania. Mbinu za usaili na hojaji zimetumika kukusanya data kutoka kwa walimu 6 wanaofundisha Kiswahili kama Lgn na wanafunzi 12 wanaojifunza lugha hiyo katika Chuo cha Maendeleo na Ushirikiano wa Kimataifa (MS TCDC) na Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA). Ukusanyaji na uchaganuzi wa data za makala hii umeongozwa na Modeli ya Elimu ya Kijamii ya Robert C. Gardner ya 2005. Mihimili miwili ya modeli hiyo imetumika kufafanua matokeo ya makala hii, kwanza, ni mhimili unaoeleza kuwa mjifunzaji wa lugha ya pili/Lgn mwenye motisha ya kujifunza lugha hiyo hutumia mikakati inayorahisisha ujifunzaji. Pili, ni mhimili unaohusu mtazamo kuhusu mazingira ya ujifunzaji wa lugha ya pili/kigeni kipengele kinachosisitiza kuwa walimu wanaofundisha lugha ya pili/kigeni wanapaswa kuyamudu mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji. Matokeo yameonesha kuwa baadhi ya walimu wanatumia lakabu kurahisisha ufundishaji wa Kiswahili kama Lgn kwa namna mbili. Mosi, ni kuwafundisha wanafunzi kulingana na tabia na uwezo unaobainishwa na lakabu zao. Pili ni kutumia lakabu kurahisisha ufundishaji wa vipengele vya sarufi. Pia, matokeo yameonesha kuwa baadhi ya wanafunzi hujifunza ...

TOP EDITORS

OPEN ACCESS JOURNALS

Dr. Afroza Begum

Lecturer, Dept. of Pharmacology and Therapeutics, Shaheed Monsur Ali Medical College & Hospital, Uttara, Dhaka-1230, Bangladesh

BEST AUTHOR

Of The Month

TRACK YOUR ARTICLE

Enter the Manuscript Reference Number (MRN)
Get Details

Contact us


EAS Publisher (East African Scholars Publisher)
Nairobi, Kenya


Phone : +91-9365665504
Whatsapp : +91-8724002629
Email : easpublisher@gmail.com

About Us


EAS Publisher (East African Scholars Publisher) is an international scholar’s publisher for open access scientific journals in both print and online publishing from Kenya. Its aim is to provide scholars ... Read More Here

*This work is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial 4.0 International License.

© 2020, All Rights Reserved | SASPR Edu International Pvt. Ltd.

Developed by JM