About Us   |   Contact Us   |  
Submission  

Upekee wa Usawiri wa Wahusika Katika Fasihi Bulibuli ya Kiswahili: Mfano Kutoka Utenzi wa Shufaka

DOI : https://doi.org/10.36349/easjehl.2024.v07i11.002
PDF
HTML
XML

Makala hii inanuia kutathmini upekee wa usawiri wa wahusika katika ushairi bulibuli wa Kiswahii kwa kurejelea. Utenzi wa Shufaka. Utenzi huu ulitungwa zamani na Hassan bin Aluwi na una jumla ya beti 285. Kwa mujibu wa Njozi (1999), utenzi huu haujavutia utafiti wa kitaaluma tangu ulipochapishwa mara ya kwanza katika jarida la Kijerumani - Zeitschriftfur Africanishen 1887. Mswada wa pekee wa utenzi huu ulipatikana katika maktaba ya German Oriental Society mjini Halle ambapo ulihifadhiwa baada ya kupelekwa hapo na Ludwig Krapf mwaka wa 1854. Knappert (1967) aliutafsiri katika lugha ya Kiingereza katika jarida la Swahili V. 37(2). Katika utangulizi wa kazi yake, Knappert aliubainisha kama utenzi muhimu kwa sababu mbili; ni wa kale, na ni mmoja kati ya sanaa sifika ya fasihi ya Kiswahili. Moja kati ya kazi iliyoshughulikia utenzi huu ni ya Njozi (1999). Amebainisha kuwa utenzi huu ni mfano wa kazi ya fasihi iliyotungwa kwa usanii wa hali ya juu ili kuibua hisi za hadhira ambayo ni sehemu muhimu sana ya utendaji wa tendi. Kipengele cha wahusika ni muhimu katika kutunga kazi yoyote ya kifasihi. Kinashirikishwa na vipengele vingine vya kifani ili kuwezesha mtunzi kutoa maudhui au ujumbe wake. Watunzi wa kazi ya kifasihi huwasawiri wahusika kisanaa ili waweze kuwakilisha watu tofautitofauti katika maisha halisi ya jamii wanayotungia. Watunzi pia hutumia mbinu mbalimbali kusawiri upekee wa sifa na hulka zinazowapambanua wahusika ili kuweza kukidhi mahitaji ya kuwa vipasa sauti vya ujumbe wanaowasilisha. Makala hii inalenga kufafanua upekee wa sifa na tabia za wahusika waliotumiwa katika Utenzi wa Shufaka. Pia tunakusudia kubainisha kuwa, ushairi hasa tenzi huwa na wahusika waliojengwa kikamilifu kwa kutumia mbinu mbalimbali za kimtindo na za lugha. Huu ni utafiti wa maktabani. Makala hii imegawika katika sehemu tatu; sehemu ya kwanza ni utangulizi; unaotoa muhtasari kuhusu Utenzi wa Shufaka, sehemu ya pili inaangazia dhana ya wahusika katika fasihi na sehemu ya tatu wahusika

TOP EDITORS

OPEN ACCESS JOURNALS

Dr. Afroza Begum

Lecturer, Dept. of Pharmacology and Therapeutics, Shaheed Monsur Ali Medical College & Hospital, Uttara, Dhaka-1230, Bangladesh

BEST AUTHOR

Of The Month

TRACK YOUR ARTICLE

Enter the Manuscript Reference Number (MRN)
Get Details

Contact us


EAS Publisher (East African Scholars Publisher)
Nairobi, Kenya


Phone : +91-9365665504
Whatsapp : +91-8724002629
Email : easpublisher@gmail.com

About Us


EAS Publisher (East African Scholars Publisher) is an international scholar’s publisher for open access scientific journals in both print and online publishing from Kenya. Its aim is to provide scholars ... Read More Here

*This work is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial 4.0 International License.

© 2020, All Rights Reserved | SASPR Edu International Pvt. Ltd.

Developed by JM