About Us   |   Contact Us   |  
Submission  

Ubainifu WA Matendo Ya Kisihiri: Mifano Kutoka Bunilizi Teule Za Fasihi Ya Kiswahili Ya Watoto

DOI : https://doi.org/10.36349/easjehl.2024.v07i02.005
PDF
HTML
XML

Sihiri ni miongoni mwa mbinu zinazotumika katika utunzi wa kazi za kifasihi zikiwamo bunilizi za watoto za fasihi mbalimbali ulimwenguni. Aidha, kumekuwa na mkanganyiko mkubwa juu ya matumizi ya matendo [ ]. ya kisihiri katika bunilizi za watoto. Wataalam wengi wa fasihi ya watoto wamechunguza fantasia kwa upekee wake bila kujadili matendo ya kisihiri kimajumui. Suala hili limesababisha kutokuchunguzwa kwa matendo mengine yanayohusisha sihiri na kuacha ombwe la maarifa juu ya matendo ya kisihiri yanayounda kazi mbalimbali za watoto na fasihi ya Kiswahili ya watoto ikiwemo. Hivyo, makala hii imebainisha na kufafanua matendo ya kisihiri yanayopatikana katika bunilizi teule za fasihi ya Kiswahili ya watoto. Ili kufanikisha lengo la makala hii, bunilizi tano za fasihi ya Kiswahili ya watoto ambazo ni Mfalme Ndevu na Masikini-Mkatakuni, Sinderela, Hadithi ya Morile, Hadithi za Kusisimua na Marimba ya Majaliwa zimechunguzwa. Data za makala hii zimekusanywa kutoka katika bunilizi teule kwa njia ya usomaji na uchambuzi matini. Nadharia ya Uhalisiajabu imeongoza ukusanyaji na uchanganuzi wa data za makala hii. Msingi wa nadharia uliotumika ni ule unaoeleza kuwa Uhalisiaajabu hutokana na muunganiko wa masuala halisi pamoja na yale yasiyo halisi. Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa bunilizi teule za fasihi ya Kiswahili ya watoto zimeundwa kwa matendo mbalimbali ya kisihiri. Matendo hayo yamegawanyika katika makundi matatu. Kundi la kwanza linahusisha matendo ya kimazingaombwe kama vile viumbe wasio binadamu kuzungumza, viumbe kujibadilisha muonekano na kuchukuwa sura na umbo la viumbe wengine, mtu kutumia vitu kujipatia mahitaji yake, vifaa visivyo rasmi kwa shughuli ya usafiri kutumika katika usafiri pamoja na fimbo kuchapa bila kushikwa na mtu. Kundi la pili linahusisha matendo ya kitabiri kama, mtu kutabiri mipango ya maadui kwa mtendwa na mtu kuteguwa kitendawili kabla ya kukisikia. Aidha, kundi la tatu limehusisha matendo ya kiganga kama vile dawa kutumika kama .......

TOP EDITORS

OPEN ACCESS JOURNALS

Dr. Afroza Begum

Lecturer, Dept. of Pharmacology and Therapeutics, Shaheed Monsur Ali Medical College & Hospital, Uttara, Dhaka-1230, Bangladesh

BEST AUTHOR

Of The Month

TRACK YOUR ARTICLE

Enter the Manuscript Reference Number (MRN)
Get Details

Contact us


EAS Publisher (East African Scholars Publisher)
Nairobi, Kenya


Phone : +91-9365665504
Whatsapp : +91-8724002629
Email : easpublisher@gmail.com

About Us


EAS Publisher (East African Scholars Publisher) is an international scholar’s publisher for open access scientific journals in both print and online publishing from Kenya. Its aim is to provide scholars ... Read More Here

*This work is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial 4.0 International License.

© 2020, All Rights Reserved | SASPR Edu International Pvt. Ltd.

Developed by JM