About Us   |   Contact Us   |  
Submission  

Ubainishaji wa vigezo vya Utoaji Wa Toponemia katika Jamii: Mfano kutoka Jimbo Dogo la Maara nchini Kenya

DOI : https://doi.org/10.36349/easjehl.2022.v05i09.002
PDF
HTML
XML

Utafiti huu wa kionomastiki ulilenga kuchanganua vigezo vya utoaji wa toponemia za shule za msingi katika jamii. Utafiti ulifanyika katika eneo la Mwimbi na Muthambi, jimboni dogo la Maara kwenye Kaunti ya Tharaka-Nithi, nchini Kenya. Nadharia ya Ujinaishaji pamoja na nadharia ya Uchanganuzi Hakiki Usemi na Matini ziliongoza utafiti huu. Data ilikusanywa kupitia mahojiano ya ana kwa ana pamoja na hojaji. Mahojiano yalimwezesha mtafiti kupata data ya kutosha na halisi moja kwa moja kutoka kwa wahojiwa. Hojaji ilimwezesha mtafiti kukusanya data kwa urahisi katika maeneo mengi na kutoka kwa sampuli kubwa. Walengwa katika utafiti huu walikuwa wakaazi wa Mwimbi na Muthambi. Usampulishaji ulifanywa kimaksudi kwa kuhusisha machifu 5 wa kata 5 za Mwimbi na Muthambi na manaibu wa chifu 25 kutoka kata ndogo 25 za eneo hili. Watawala hao walichaguliwa kwa sababu walikuwa wenyeji wa eneo la utafiti na iliaminika kuwa wangetoa habari kamilifu kuhusu maswali ya utafiti. Sampuli nyingine ya Wazee 20 wenye umri wa miaka 70 na zaidi ilichaguliwa kimakusudi kwa kutumia mbinu ya kimtandao ili kutoa habari kuhusu michakato ya uundaji wa toponemia za shule za msingi katika eneo la Mwimbi na Muthambi. Sampuli ya wazee ilipatikana kwa urahisi kwa kuwa walikuwa wakipokea marupurupu maalum kutoka kwa serikali, na hivyo walijulikana katika vijiji vyao. Uchambuzi na uwasilishaji wa data ya utafiti huu ulitumia mkabala wa kimaelezo kulingana na madhumuni na swali la utafiti. Utafiti huu ulibainisha kuwa toponemia hutolewa kwa kuzingatia vigezo vya kimaumbile, kiuchumi na kijamii. Matokeo ya utafiti huu yatatoa marejeleo muhimu kwa watafiti wa baadaye watakaoshughulikia vipengele vya onomastiki katika lahaja ya Kimwimbi na Muthambi na lugha nyinginezo.

TOP EDITORS

OPEN ACCESS JOURNALS

Dr. Afroza Begum

Lecturer, Dept. of Pharmacology and Therapeutics, Shaheed Monsur Ali Medical College & Hospital, Uttara, Dhaka-1230, Bangladesh

BEST AUTHOR

Of The Month

TRACK YOUR ARTICLE

Enter the Manuscript Reference Number (MRN)
Get Details

Contact us


EAS Publisher (East African Scholars Publisher)
Nairobi, Kenya


Phone : +91-9365665504
Whatsapp : +91-8724002629
Email : easpublisher@gmail.com

About Us


EAS Publisher (East African Scholars Publisher) is an international scholar’s publisher for open access scientific journals in both print and online publishing from Kenya. Its aim is to provide scholars ... Read More Here

*This work is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial 4.0 International License.

© 2020, All Rights Reserved | SASPR Edu International Pvt. Ltd.

Developed by JM