About Us   |   Contact Us   |  
Submission  

Ushairi WA Kiganda Unavyoweza Kuchangia Na Kuendeleza Ushairi WA Kiswahili Kimtindo Na Kimaudhui: Mfano WA Ufundishaji Nchini Uganda

DOI : https://doi.org/10.36349/easjehl.2022.v05i04.003
PDF
HTML
XML

Wanafunzi wengi nchini Uganda wanachukulia utanzu wa ushairi wa Kiswahili kuwa mgumu na wanapata ugumu katika kujifunza ushairi wa Kiswahili. Ushairi wa Kiganda umekuwa unatendwa vizuri katika mtihani wa kitaifa. Upande wa Kiswahili, kuna ugumu katika ujifunzaji wa ushairi wa Kiswahili na ugumu huu umesababisha matokeo mabaya katika mtihani wa kitaifa katika somo la ushairi wa Kiswahili nchini Uganda. Wanafunzi hawa husomea katika mandhari sawa. Hili linazua swali: kwa nini wanafunzi wanaofanya mtihani wa ushairi wa Kiganda watende vizuri kuliko wanafunzi wa ushairi wa Kiswahili? Makala hii itaweka wazi mambo ambayo ushairi wa Kiswahili waweza kukopa kutoka ushairi wa Kiganda na kujiendeleza. Madhumuni ya makala hii yatakuwa: Kudadavua jinsi ushairi wa Kiganda unaweza kusahilisha mtindo katika ushairi wa Kiswahili kupitia ufunzaji na ujifunzaji na kutathimini jinsi ushairi wa Kiganda unaweza kukuza maudhui katika ushairi wa Kiswahili kupitia ufunzaji na ujifunzaji. Mashairi yalikusanywa kutoka diwani mbili za Kiswahili na mbili za Kiganda. Mashairi 60 yalikusanywa yaani 30 ya Kiganda na 30 ya Kiswahili na 15 yalichaguliwa kutoka kila lugha kwa kutumia uteuzi nasibu. Mashairi yalitolewa kwenye diwani za Kiswahili; “Malenga wa ziwa kuu” na “Malenga wa karne moja” na za Kiganda; “Ab’Oluganda ab’Enda emu” na “Balya n’ensekeezi”. Makala hii unafafanua jinsi mwalimu wa ushairi wa Kiswahili anavyoweza kuhamisha maarifa kutoka ushairi wa Kiganda hadi wa Kiswahili. Utamsaidia kuendeleza ushairi wa Kiswahili kuhamisha maarifa ya ujifunzaji na ufunzaji kutokana na ushairi wa Kiganda ili kusahilisha ujifunzaji wa ushairi wa Kiswahili.

TOP EDITORS

OPEN ACCESS JOURNALS

Dr. Afroza Begum

Lecturer, Dept. of Pharmacology and Therapeutics, Shaheed Monsur Ali Medical College & Hospital, Uttara, Dhaka-1230, Bangladesh

BEST AUTHOR

Of The Month

TRACK YOUR ARTICLE

Enter the Manuscript Reference Number (MRN)
Get Details

Contact us


EAS Publisher (East African Scholars Publisher)
Nairobi, Kenya


Phone : +91-9365665504
Whatsapp : +91-8724002629
Email : easpublisher@gmail.com

About Us


EAS Publisher (East African Scholars Publisher) is an international scholar’s publisher for open access scientific journals in both print and online publishing from Kenya. Its aim is to provide scholars ... Read More Here

*This work is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial 4.0 International License.

© 2020, All Rights Reserved | SASPR Edu International Pvt. Ltd.

Developed by JM