About Us   |   Contact Us   |  
Submission  

Visababishi Vya Uhusiano Wa Kimahaba Na Mimba Za Utotoni Kwa Mujibu Wa Waandishi Wa Hadithi Fupi Teule Za Kiswahili

DOI : https://doi.org/10.36349/easjehl.2021.v04i10.001
PDF
HTML
XML

Dhima ya fasihi ya Kiswahili hasa utanzu wa hadithi fupi katika ulimwengu wa leo haiwezi kupuuzwa kamwe. Hii ni kwa sababu fasihi ni kioo cha jamii cha kutazamia mambo mbalimbali yanayofanyika katika jamii pana. Utafiti huu unajadili visababishi vya uhusiano wa kimahaba na mimba za utotoni kwa mujibu wa hadithi fupi teule za Kiswahili. Uhusiano wa kimahaba na mimba za utotoni ni suala nyeti linaloangazia ukiukaji wa haki za watoto kwa mujibu ya katiba ya Kenya (2010) na kuathiri watoto wengi wanaofaa kuwa shuleni. Baadhi ya visababishi vya suala hili kwa mujibu wa utafiti huu ni pamoja na ubakaji, shinikizo la wanarika, ukiukaji wa maadili, ulipizaji kisasi, uhitaji, ulevi, mazingira mabaya na kutowajibika kwa wazazi na walezi. Hadithi fupi teule zilizochanganuliwa zilitolewa kwenye diwani za Damu Nyeusi na Hadithi Nyingine (2007), Kurudi Nyumbani na Hadithi Nyingine (2007), Alidhani Kapata na Hadithi Nyingine (2007) na Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyingine (2016). Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Mwitikio wa Msomaji ambayo hunuia kubainisha na kufafanua kadhia zinazomkutanisha msomaji na kazi ya fasihi na kumpa msomaji uhuru wa kufasiri kazi ya fasihi apendavyo. Waasisi na watetezi wakuu wa nadharia hii ni pamoja na Wolfgang Iser (1974,1978), Stanley Fish (1980) na James Tompkins (1980). Umuhimu wa utafiti huu ni kuwa utauhamasisha umma kuhusu umuhimu wa fasihi ya Kiswahili katika jamii, ikiwemo kuyachanganua masuala-ibuka na masuala-nyeti na kutafuta suluhu kwa matatizo ya kijamii. Aidha, utawahamasisha watetezi wa haki za watoto kuhusu visababishi vya uhusiano wa kimahaba na mimba za utotoni nchini Kenya na kwingineko ulimwenguni, pamoja na utatuzi wake.

TOP EDITORS

OPEN ACCESS JOURNALS

Dr. Afroza Begum

Lecturer, Dept. of Pharmacology and Therapeutics, Shaheed Monsur Ali Medical College & Hospital, Uttara, Dhaka-1230, Bangladesh

BEST AUTHOR

Of The Month

TRACK YOUR ARTICLE

Enter the Manuscript Reference Number (MRN)
Get Details

Contact us


EAS Publisher (East African Scholars Publisher)
Nairobi, Kenya


Phone : +91-9365665504
Whatsapp : +91-8724002629
Email : easpublisher@gmail.com

About Us


EAS Publisher (East African Scholars Publisher) is an international scholar’s publisher for open access scientific journals in both print and online publishing from Kenya. Its aim is to provide scholars ... Read More Here

*This work is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial 4.0 International License.

© 2020, All Rights Reserved | SASPR Edu International Pvt. Ltd.

Developed by JM