About Us   |   Contact Us   |  
Submission  

Mitindo Ya Ujifunzaji Lugha Ya Pili Katika Kufanikisha Ujifunzaji Wa Kiswahili Kama Lugha Ya Biashara Jijini Kampala, Uganda

DOI : https://doi.org/10.36349/easjehl.2021.v04i06.003
PDF
HTML
XML

Shughuli za biashara nchini Uganda zilianza zama za kale wakati wa ujio wa wakoloni na usambazaji wa Kiswahili. Kiswahili kilisambaa Uganda kupitia njia mbalimbali moja wapo ikiwa ni biashara. Kimsingi, maingiliano ya jamii zenye tamaduni na lugha mbalimbali hutokana na ushirikiano katika biashara na shughuli nyinginezo za kijamii. Shughuli hizo huzua haja za kuwepo kwa lugha moja itakayoweza kuwaunganisha watu wenye tamaduni na lugha mbalimbali. Hivyo basi, uendelezaji wa biashara unakuwa mgumu bila matumizi ya lugha inayoeleweka na wengi. Kutokana na hali hii, kujifunza Kiswahili kama lugha ya biashara hakuepukiki. Madhumuni ya utafiti ni kuelezea mitindo anuwai ya ujifunzaji wa lugha ya pili, na jinsi wafanyabiashara wametumia mitindo hiyo kujifunza Kiswahili kama lugha ya biashara kwa kuongozwa na nadharia ya Gardener ya 1985. Data ilikusanywa kutoka nyanjani miongoni mwa wafanya biashara jijini Kampala, Uganda. Eneo la utafiti lilikuwa ekedi ya Mukwano na soko la Kikuubo nchini Uganda na ulihusisha eneo la kitaaluma la ujifunzaji lugha ya pili.Idadi lengwa ilihusisha wafanya biashara waliokuwa wakiendeleza biashara tofauti tofauti katika maeneo hayo ya ekedi ya Mukwano na soko la Kikuubo nchini Uganda.Usampulishaji dhamirifu ulizingatiwa katika uteuzi wa sampuli ya wafanya biashara 100 waliochunguzwa katika harakati za kununua na kuuza.Data ilikusanywa kupitia mbinu ya kuangalia na majadiiano kupitia usaili.Data hiyo ilipangwa na kuchujwa kulingana na madhumuni ya utafiti.Dondoo zilizokusanywa kutoka kwa wasailiwa zilipewa kodi zufuatazo:Ms1=Msailiwa 1,Ms2 kumaanisha msailiwa wa pili kwa mfuatano huo.

TOP EDITORS

OPEN ACCESS JOURNALS

Dr. Afroza Begum

Lecturer, Dept. of Pharmacology and Therapeutics, Shaheed Monsur Ali Medical College & Hospital, Uttara, Dhaka-1230, Bangladesh

BEST AUTHOR

Of The Month

TRACK YOUR ARTICLE

Enter the Manuscript Reference Number (MRN)
Get Details

Contact us


EAS Publisher (East African Scholars Publisher)
Nairobi, Kenya


Phone : +91-9365665504
Whatsapp : +91-8724002629
Email : easpublisher@gmail.com

About Us


EAS Publisher (East African Scholars Publisher) is an international scholar’s publisher for open access scientific journals in both print and online publishing from Kenya. Its aim is to provide scholars ... Read More Here

*This work is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial 4.0 International License.

© 2020, All Rights Reserved | SASPR Edu International Pvt. Ltd.

Developed by JM